TANZU
ZA FASIHI ANDISHI
RIWAYA (NATHARI)
USHAIRI (NUDHUMU)
TAMTHILIYA (SANAA ZA MAONYESHO)
FANI NA MAUDHUI KATIKA FASIHI
Fani
na maudhui katika fasihi ndio maumbo mawili makuu yanayobeba sanaa hii.
FANI
Fani
ni ufundi unaotumiwa na msanii katika kufikisha ujumbe uliokusudiwa, fani sio
ujumbe bali ni mfano wa kipaza sauti kinachotumika kufikisha ujumbe.
VIPENGELE VYA FANI
Fani
inavipengele vingi, kila kipengele kina husika kipekee kwa kutofautiana na
kipengele kingine.
Vipengele vya fani ni pamoja na;
a) Muundo
Kipengele
hiki hutumiwa kueleza mpangilio wa kazi ya kifasihi. Kwa ufupi kwenye kipengele
cha muundo tunaangalia umbo la kazi ya fasihi, mfano kazi yaweza kugawanywa
katika sura mbalimbali, sura hizi ndizo ujenga muundo.
b) Mtindo
Williady
(2015) mtindo ni mbinu za kipekee zinazomtofautisha msanii mmoja na mwingine.
Mfano katika fasihi simulizi kipengele cha nyimbo hadhira inaweza kusikia wimbo
kwa mara ya kwanza na kutambua wimbo huo umeimbwa na nani bila ya kuambiwa na
mtangazaji, hii huweza kutokea pindi mwimbaji mashuhuri anayetumia mtindo wa
peke yake katika sauti na mpangilio wa mashairi anapotoa wimbo mpya. Huu ndio
huitwa mtindo. Katika fasihi andishi mtindo unaweza kujitokeza kwa njia za
kipekee za mtunzi katika matumizi ya lugha, methali na misemo, msuko na
mpangilio wa vina na mizani katika ushairi.
c) Mandhari
Williady
(2015) Mandhari ni eneo au mazingira ya kweli au yakubuni ambayo hutumiwa na
mwandishi katika kuwajenga wahusika na uhusika wao.
d) Matumizi ya Lugha
Williady
(2015) Matumizi ya lugha ni ustadi wa msanii katika kutumia lugha itakayoleta
mvuto kwa wasomaji au wasikilizaji wa kazi ya fasihi.
Katika
kutumia lugha msanii lazima azingatie kipengele cha uteuzi wa maneno
yanayoendana na hadhira yake, maneno hayo ndiyo yatakayoleta mfungamanisho
katika ya msanii, hadhira na ujumbe uliokusudiwa.
e) Matumizi ya tamathali za semi(usemi)
Williady
(2015) Tamathali maanayake ni neon moja au kifungu cha maneno kilicho
sukwasukwa na kufichwa maana.
Baadhi
ya tamathali za semi katika Kiswahili ni pamoja na;
Tashibiha,
sitiari, tafsida, tashihisi, chuku, kinaya,dhihaka, mbalagha,tabaini
f) Mbinu nyingine za kisanaa
Hapa
huwa na mchanganyiko wa mbinu kadhaa katika usimulizi na silazima mbinu hizo
zitumike zote kwa wakati mmoja. Mfano wa mbinu hizo ni pamoja na;
Takriri, kuchanganya ndimi, tanakali sauti, taswira, lakabu, nahau na misemo
Takriri, kuchanganya ndimi, tanakali sauti, taswira, lakabu, nahau na misemo
e) Wahusika
Williady
(2015) wahusika ni viumbe hai au viumbe ambao si hai wanaobebeshwa majukumu na
msanii ili kuwafikishia hadhira ujumbe uliokusudiwa.
MAUDHUI KATIKA FASIHI SIMULIZI
(williady:
2015) Maudhui ni jumla ya mawazo anayoyazungumzia msanii au mtunzi katika kazi
ya fasihi.
Maudhui
hujumuisha vipengele mbalimbali, kama vile;Dhamira, ujumbe, falsafa, mafunzo,
migogoro na mtazamo.
TANBIHI:
Kuna baadhi ya wataalamu wa lugha wanakiweka kipengele cha migogoro upande wa
fani na kunabaadhi wanakiweka kipengele hiki upande wa maudhui. Mimi nakiweka
upande wa maudhui kwa kuwa migogoro inabeba kwa kiasi kikubwa ujumbe kuliko
ufundi.
DHAMIRA
Dhamira
ni shabaha kuu ya mtunzi wa kazi ya fasihi. Shabaha hii ukusudiwa ni nani
wakumlenga nayo. Msanii anaweza kuwalenga kimaudhui watoto, wanawake, wasomi au
watu wote katika jamii. Shabaha hii yaweza kuandikwa au kutongolewa kwa mdomo
ikiwa na lengo la kupongeza, kuhimiza, kushauri, kutoa taarifa na kukosoa.
UJUMBE
Ujumbe
ni mawazo yanayotokana na dhamira, mawazo haya yaweza kujitokeza waziwazi au
kwa kificho.
FALSAFA
Falsafa
ni hekima hekima ya mtunzi. Mtunzi huamini kuwa kupitia imani hii jamii
inaweza kupata suluhisho la matatizo yanayowakabili. Kwa mfano shekhe Shaaban
Robert aliamini kuwa kila mwanajamii akiwa na utu basi haki na upendo
vitapatikana kirahisi.
MAFUNZO
Mafunzo
ni nasaha anazotoa mtunzi ambazo huifundisha hadhira maadili Fulani. Maana ya
mafunzo hutegemea namna hadhira inavyofasili nasaha hizo.
MIGOGORO
Migogoro
ni misuguano au mikinzano ama kutoelewana kati ya pande mbili au zaidi ndani ya
kazi za fasihi.
AINA ZA MIGOGORO
Mgogoro kati ya mtu na mtu
Mgogoro kati ya mtu na jamii
Mgogoro kati ya jamii na jamii
Mgogoro wa nafsi
VI. MTAZAMO
Mtazamo
na jinsi mwandisi anavyotazama na kuyachukulia matukio katika ulimwengu na
athari zake kwa wanajamii. Mfano waandishi wengi wa mashairi wanamtazamoa huu
“Kuibuka kwa maovu mengi duniani kwasasa ni matokeo ya binadamu kuasi
dini.
mawasiliano:
0657882566
0742508002